Wapi uwekeze, Kenya au Tanzania?

Watanzania wengi waishio nje ya nchi wanaotaka kuwekeza hapa Afrika Mashariki mara nyingi hujiuliza, kati ya Tanzania na Kenya, nchi ipi inafaa zaidi kwa uwekezaji? 

Nchi zote zina miji yenye shughuli nyingi, na masoko yanayotamanisha. Lakini kwa wale wanaotafuta faida ya muda mrefu, yenye hasara kidunchu, na fursa ambazo bado hazijagunduliwa na wengi, Tanzania mara nyingi inachukua nafasi ya kwanza.

Sisi elegant.africa, tunawasaidia wawekezaji kuelewa soko la uwekezaji wa majengo Afrika mashariki (Real Estate Market). Tumekuandalia dondoo zinazoonyesha kwa nini Tanzania ni chaguo sahihi zaidi kuliko Kenya. 

Fuatana nasi: 

1. Sheria zinazoeleweka
Kenya imekuwa na migogoro mingi sana ya ardhi, na mabadiliko ya sheria mara kwa mara. Hii mara nyingi husababisha ucheleweshaji wa miradi na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji.

Tanzania kwa upande mwingine, imepunguza kero hizi kwa kuweka taratibu nzuri za kuharakisha upataji vibali vya uwekezaji. Wafanyabiashara wa kigeni wanaweza kupata mikataba ya muda mrefu hadi miaka 99. 

2. Gharama za Kuanzia
Bei za ardhi na ujenzi Kenya, hasa Nairobi, ziko juu sana, ikimaanisha kuanza ni ghali sana na faida inaweza kuwa ndogo kwa wawekezaji wapya.

Dar es Salaam bado inatoa fursa za kumwaga.  Ardhi ni bei nafuu zaidi kuliko Kenya, na gharama za ujenzi si za kutisha. Unaweza kuanza na mtaji mdogo na ukapata faida. 

3. Urahisi wa kupata soko
Nairobi, hasa kwa apartments za gharama kubwa, tayari soko limejaa, hivyo nafasi kwa wawekezaji wapya ni chache. 

Ila, Kigamboni na maeneo mengine ya Dar es Salaam bado hayajajaa. Idadi ya watu inaongezeka, lakini miradi iliyopo sasa haijakidhi mahitaji. Wawekezaji wapya bado wana nafasi ya kujenga na kupata wateja wengi tu wa kupangisha. 

4. Mazingira Rahisi ya Uwekezaji
Wawekezaji wa Tanzania wana njia za wazi na rahisi za kumiliki mali kwa mikataba ya muda mrefu. Migogoro ya kisheria ni michache ikiwa unafuata utaratibu. Hii ni tofauti na Kenya, ambapo ada za kisheria na utatuzi wa migogoro zinaweza kula hadi 5–10% ya thamani ya uwekezaji wako. 

Hitimisho

Hauhitaji pesa nyingi sana kuanza kuwekeza Tanzania. Hii ndo faida yake kubwa ukilinganisha na Kenya.  

Iwapo unahitaji mwongozo wa uwekezaji, tupo tayari kukusaidia kufanya utafiti, kuchagua eneo, kubuni mradi (architectural design) na kukujengea kwa ubora wa hali ya juu sana. 

Wasiliana nasi kupitia: 

📩 designers@elegant.africa
📲 +255 745 749 973 au +255 787 165 837 au +250 789 902 748 (Whatsapp)

 

 

 

 

 

Rudi Nyuma

Andika maoni yako